• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mazungumzo ya ustaarabu ya Asia kufunguliwa tarehe 15 Mei mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2019-05-09 18:44:59

    Ofisi ya habari ya baraza la serikali la China imesema mkutano wa mazungumzo ya ustaarabu ya Asia utafunguliwa tarehe 15 Mei mjini Beijing. Rais Xi Jinping wa China atahudhuria sherehe hiyo na kutoa hotuba. Viongozi wengine kutoka Cambodia, Ugiriki, Singapore, Sri Lanka, Armenia, Mongolia, na wakuu wa mashirika ya kimataifa ikiwemo UNESCO watahudhuria mkutano huo, na wawakilishi kutoka nchi 47 za Asia na nchi nyingine pia watashiriki kwenye shughuli husika.

    Ajenda ya mkutano huo ni mawasiliano ya ustaarabu wa Asia na jumuiya yenye mustakabali wa pamoja. Aidha China inatarajia kunufaika zaidi na kuendelea na mafanikio ya ustaarabu ya watu wa Asia na ulimwengu, kukuza mawasiliano na kujifunza kwa pamoja kwa nchi tofauti na ustaarabu tofauti, kuendeleza zaidi maendeleo ya ustaarabu wa binadamu, na kuendelea kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako