Atwoli amesema mishahara ya wabunge inapasa kuongezwa ili kuwawezesha kutosheleza matakwa ya wananchi ambao huwaomba pesa kila mara.
Atwoli amesema tabia ya Wakenya ya kuwaomba wabunge pesa kila mara ndiyo imechochea ufisadi nchini Kenya. Ameongeza kuwa wabunge wengi wanalazimika kutoa fedha nyingi kwa wananchi wakati wanapopata matatizo kama vile misiba na hata magonjwa. Kinara huyo wa COTU alisema kuna baadhi ya wabunge ambao hutumia kati ya Sh300,000 na Sh600,000 kila wiki wanapotembelea maeneobunge yao; pesa ambazo wanatarajiwa kutoa kutoka kwa mishahara yao. Kiongozi huyo wa Cotu alitoa wito kwa Wakenya kushiriki katika shughuli za kuwaletea mapato kama vile kilimo badala ya kutegemea viongozi wao kwa mahitaji yao ya kila siku. Kauli hiyo inajiri baada ya wabunge na maseneta kujitengea shilingi bilioni 936 kama marupurupu ya nyumba iliyopendekezwa na Tume ya Huduma za Bunge (PSC) 2018.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |