• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kaunti ya Nandi, Kenya yadaiwa kupoteza Sh2.3b

    (GMT+08:00) 2019-05-09 20:29:21
    Kaunti ya Nandi inadaiwa kupoteza jumla ya shilingi bilioni 2.3 pesa za umma.

    Baadhi ya wabunge wa seneti wameitaka idara ya Upelelezi wa Jinai kuchunguza madai hayo na kuwachukulia hatua wahusika waliopelekea kutoweka kwa fedha hizo.

    Kauli hiyo inakuja baada ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Edward Ouko kuibua maswali kuhusu kupotea kwa jumla ya Sh2.3 bilioni tangu Gavana Stephen Sang' kuingia mamlakani mwaka wa 2017. Pesa hizi zimepotea katika idara sita za kaunti hiyo.

    Maseneta hao wamedai kuwa hatua ya Bw Sang' ya kuwasimamisha kazi maafisa 16 wa serikali yake, wakiwemo mawaziri watatu ni hatua ya kujiondolea lawama ilhali yeye ndiye chanzo cha uovu huo katika serikali yake. Mwaka 2018 kaunti hiyo ilitumia shilingi milioni 2.4 kukodi helikopta iliyotumiwa na ofisi ya Gavana kwenda kujivinjari katika Mbuga ya Kitaifa ya Maasai Mara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako