• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watumishi 8,400 waajiriwa na serikali Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-05-09 20:29:38
    Bunge la Tanzania limeelezwa kuwa kwa mwaka wa fedha 2017/18 na 2018/19, serikali imeajiri jumla ya watumishi 8,444 wa kada mbalimbali za afya kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

    Hayo yalielezwa bungeni na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Josephat Kandege, alipokuwa akijibu maswali bungeni.

    Bunge lilikuwa likitaka kujua kama hospitali na vituo vya afya nchini humo vinakidhi vigezo vya utoaji huduma kwa wagonjwa.

    Kandege alisema serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya afya, kuajiri wataalam, kununua dawa, vitendanishi na vifaa tiba ili kuhakikisha vituo vya kutolea huduma vinakidhi viwango vinavyohitajika.

    Aidha, alisema ili kuboresha viwango vya utoaji huduma za afya nchini humo katika mwaka wa fedha 2017/18 na 2018/19 serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 285.17 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali 67 za Halmashauri.

    Kadhalika, alisema kwa mwaka wa fedha 2019/20 serikali imetenga Sh. bilioni 23.9 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali mpya 27 za wilaya na ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya 52.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako