• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Liu He awasili Washington kuhudhuria duru ya 11 ya mazungumzo ya biashara kati ya China na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-05-10 07:50:36

    Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He, ambaye pia ni kiongozi wa ujumbe wa China kwenye mazungumzo ya biashara kati ya China na Marekani, jana aliwasili mjini Washington kuhudhuria duru ya 11 ya Mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu masuala ya uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili.

    Akiongea na wanahabari baada ya kuwasili, Bw. Liu He amesema amekwenda na nia njema, akitumai kuwa ataweza kubadilishana maoni na upande wa Marekani kwa njia ya mantiki na udhati katika hali maalumu ya sasa. Amesema China inaona kuongeza ushuru wa forodha sio ufumbuzi wa mgogoro, na hakutanufaisha pande zote mbili za China na Marekani, wala dunia nzima kwa ujumla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako