• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yalikosoa Baraza la chini la Bunge la Marekani kupitisha miswada inayohusu Taiwan

    (GMT+08:00) 2019-05-10 09:55:01

    Baraza la chini la Bunge la Marekani Jumanne lilipitisha miswada ya "Sheria ya Uhakikisho wa Taiwan" na "Kutambua upya ahadi ya Marekani kwa Taiwan na kutekeleza Sheria ya Uhusiano na Taiwan". Jumuiya ya kimataifa imefuatilia kwa karibu hatua hiyo, na kuona kitendo hicho cha Marekani kimeingilia kati mambo ya ndani ya China, na kitahujumu vibaya uhusiano kati ya China na Marekani, na kuyumbisha amani na utulivu kwenye mlango bahari wa Taiwan.

    Naibu msemaji wa Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Farhan Haq amesema, Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono kithabiti Kanuni ya China Moja, kwa mujibu wa maazimio husika, likiwemo Azimio lililopitishwa mwaka 1971 kwenye Kikao cha Baraza kuu la Umoja huo.

    Mtaalamu wa masuala ya China na Afrika wa Kenya Bw. Edhurley Cavens amesema, kanuni ya China Moja ni msingi muhimu wa kisiasa kwa China kukuza mahusiano na nchi mbalimbali duniani, na suala la Taiwan ni suala muhimu zaidi na nyeti zaidi katika uhusiano wa China na Marekani, kwa hivyo Marekani kutumia suala hilo kama silaha dhidi ya China kamwe hakuwezi kufikia lengo lake.

    Wataalamu kutoka nchi nyingi zikiwemo Russia, Indonesia, Malaysia, Cuba, Brazil, Argentina, Mexico, Nigeria na Misri pia wametoa maoni ya kuikosoa hatua hiyo ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako