• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatangaza kujibu hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China

    (GMT+08:00) 2019-05-10 14:00:41

    China imetoa taarifa ikieleza kusikitishwa na hatua ya Marekani ya kuongeza rasmi ushuru wa forodha dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 zinazoingia nchini humo kutoka asilimia 10 hadi 25, na kusema italazimika kuchukua hatua za lazima za kujibu.

    Taarifa imesema duru ya 11 ya mazungumzo ya ngazi ya juu ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani inafanyika mjini Washington, na China inaitaka Marekani iende sambamba na China na kufanya juhudi za pamoja ili kutatua matatizo yaliyopo kwa njia ya ushirikiano na mashauriano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako