• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China yaathiri maslahi ya China na pia kujiharibu

    (GMT+08:00) 2019-05-10 16:51:53

    Marekani imetangaza kuongeza ushuru kwa bidhaa za China zinazouzwa nchini humo zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kuanzia leo saa sita na dakika 1 kwa saa za hapa Beijing, huku China ikitangaza hatua ya kuijibu siku hiyo hiyo saa sita na dakika 3 kwa saa za Beijing.

    Vita ya biashara kati ya pande hizi mbili imepamba moto kwa mara nyingine tena, hali ambayo inasikitisha watu. Chanzo cha hali hii ni uelewa mbaya wa Marekani wa msimamo na vitendo vyenye msimamo wa dhati vya China, kushikilia kanuni yake ya "kutoa kipaumbele cha Marekani", na kutaka faida bila ya msingi huku ikiweka shinikizo bila ukomo, hatua ambayo imekwenda kinyume na kanuni ya mazungumzo ya kuheshimiana, usawa na kunufaishana.

    Mazungumzo yanategemea misimamo ya pande zote mbili. Upande wa China umeonesha udhati wake kwa hatua halisi, lakini pia unahitaji juhudi za pamoja za Marekani zinazoelekea kwa upande mmoja. Mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja,huku China ikifahamu vizuri tabia ya Marekani, wakati huo huo, Marekani pia imetambua wazi kanuni na msimamo wa China, kwamba China haipendi vita lakini pia haina woga ya kufanya vita, na itabidi kuvifanya vita kama ikilazimika. China inapenda kutatua migogoro ya kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili kwa njia ya ushirikiano lakini kwa sharti kwamba haipaswi kuathiri maslahi muhimu ya nchi na maslahi ya kimsingi ya wananchi wake.

    Watu wanapaswa kutambua kwamba, Marekani imeacha majukumu yake ya kimataifa kwa Shirika la Biashara Duniani WTO, wakati pande hizo mbili zikikaribia kufikia makubaliano ya kihistoria, na kuongeza ushuru kwa makusudi, hatua ambayo ni kinyume na kanuni ya biashara ya pande nyingi, na itaathiri vibaya zaidi maslahi ya pande mbili za China na Marekani na hata dunia nzima, na kupingwa vikali na jamii ya kimataifa wakiwemo Wamarekani wenyewe. Mkurugenzi wa Shirikisho la wafanyabiashara la Marekani Bw. Thomas J. Donohue ameeleza bayana kwamba, haungi mkono uamuzi wa Marekani wa kufanya vita ya kibiashara kwa njia ya kuongeza ushuru, kwani ushuru unatozwa na familia na kampuni za Marekani badala ya wageni.

    Jaribio la Marekani la kuzuia hatua ya kujiendeleza ya China kwa njia ya kuongeza ushuru halitafanikiwa. Katika mwaka mmoja uliopita, China imekabiliana na changamoto kwa njia mwafaka, huku uwezo wa ukuaji wa uchumi, jamii hata imani ya wananchi ya kukabiliana na shinikizo ukizidi kuongezeka. Hivi sasa ishara mbalimbali chanya za kuisaidia China zimeonekana, na China itakabiliana na changamoto mbalimbali kwa imani kubwa zaidi. Pia China italeta fursa nyingi za maendeleo kwa njia ya kuongeza nguvu katika mchakato wa mageuzi, na kuhimiza ufunguaji mlango kwenye kiwango cha juu zaidi ili kuhimiza maendeleo ya uchumi kupata maendeleo yenye kiwango cha juu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako