• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Yi ahudhuria ufunguzi wa mkutano wa baraza la kimataifa la ushirikiano kati ya China, Japani na Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2019-05-10 18:13:56

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi amehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa mkutano wa baraza la kimataifa la ushirikiano kati ya China, Japani na Korea Kusini mwaka 2019 unaofanyika hapa Beijing.

    Bw. Wang amesema, mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 20 ya ushirikiano kati ya China, Japani na Korea Kusini, na ushirikiano huo umesimama katika mwanzo mpya wa kihistoria. Katika miaka 20 iliyopita, ushirikiano kati ya nchi hizo tatu umepata maendeleo makubwa na kutoa mchango mkubwa katika kunufaisha maslahi ya watu wa nchi hizo, kulinda amani na utulivu wa Asia na kuhimiza maendeleo na ustawi wa dunia.

    Bw. Wang pia amesema, ushirikiano huo umefika katika kipindi cha kukua na kukabiliwa na fursa mpya. China, ikiwa nchi mwenyekiti wa ushirikiano kati ya nchi hizo tatu, inapenda kufanya juhudi pamoja na Japani na Korea Kusini kuinua ushirikiano huo katika kiwango cha juu zaidi na kuufanya kuwa injini yenye nguvu ya kuhimiza maendeleo ya Asia, pia kuwa kiongozi wa kuhimiza uchumi wa uwazi na kuwa nguvu kuu ya kulinda kanuni za uhusiano wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako