• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema makubaliano ya pande zote ya suala la nyuklia la Iran yanapaswa kutekelezwa kikamilifu na kwa ufanisi

    (GMT+08:00) 2019-05-10 19:36:55

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesisitiza kuwa, makubaliano ya pande zote ya suala la nyuklia la Iran ni ya pande nyingi na yameidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Amesema makubaliano hayo ni muhimu kwa mfumo wa kutoeneza silaha za nyuklia duniani na amani na utulivu kwenye eneo la Mashariki ya Kati, kwa hiyo yanapaswa kutekelezwa kikamilifu kwa ufanisi.

    Amesema Marekani imejitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran na kuiwekea vikwazo Iran kwa upande wake mmoja na kuingilia mambo ya ndani ya Iran, hivyo kusababisha hali ya wasiwasi ya hivi sasa. China inatoa wito kwa pande husika ziwe na uvumulivu, kuimarisha mawasiliano, kuunga mkono na kulinda makubaliano hayo, ili kuepuka kuchochea hali ya wasiwasi zaidi. China inapenda kuendelea kutekeleza ahadi yake ya kulinda na kutekeleza makubaliano hayo pamoja na pande husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako