• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KRA yamulika wafanyabiashara wa mitandaoni

    (GMT+08:00) 2019-05-10 19:47:29
    Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru NchiniKenya (KRA) imetaka wafanyabiashara wanaondesha shughuli zao mitandaoni kulipa ushuru ikionya baadhi yao wanaokwepa kwamba wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

    KRA imesema imebaini kuwa baadhi ya watu wanaoendesha biashara mitandaoni huwa hawalipi ushuru wala kujaza fomu za kuonyesha ushuru wanaolipa kwa mapato yao kila mwaka. Imesema watu hao sharti walipe ushuru la sivyo wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Adhabu ya kutowasilisha taarifa ya ulipaji ushuru ni Sh20,000 kwa mwaka.

    KRA ilisema wafanyabiashara mitandaoni wanahitajika kuwasilisha fomu za ushuru na kulipa ushuru zote ikiwemo ile ya ziada ya thamani (VAT), ushuru wa kampuni, ushuru za bidhaa kati ya aina zingine zinazolipwa na wafanyabiashara wa kawaida. KRA inataraji kwamba zaidi ya walipa ushuru 4 milioni watawasilisha taarifa zao za ulipaji ushuru (tax returns) kwa mfumo wa iTax kufikia Juni 30, 2019. Mwaka 2018 zaidi ya walipa ushuru 3.2 milioni waliwasilisha taarifa zao za ulipaji ushuru kwa mfumo huo wa kimtandao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako