• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapewa 5 uzalishaji mchele bora

    (GMT+08:00) 2019-05-10 20:04:28

    Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazozalisha mchele mzuri na msafi na ambao una thamani ukilinganisha na mchele unaozalishwa Msumbiji, Kenya, Rwanda na Burundi.

    Pia imetajwa kuwa nchi yenye idadi kubwa ya wanawake wanaozalisha kwa wingi zao hilo ambapo huzalisha tani 5-8 kwa hekta.

    Hayo yalibainishwa na mtaalamu wa kilimo kutoka Jimbo la Zambezia, Msumbiji, Jaime Gado, alipotembelea Tanzania akiwa na timu ya wataalamu saba wa mpunga na mmoja kutoka Japan, kwa lengo la kubadilishana ujuzi na kujifunza kutoka kwa wakulima wa Tanzania kuhusu namna ya kuzalisha mpunga bora.

    Gado amesema mbali na changamoto ya kuwa na mashine zilizochakaa na ubovu wa miundombinu ikiwemo barabara, bado mkulima wa Tanzania amekuwa na hai ya kuzalisha mpunga bora.

    Naye mtaalamu kutoka Tanzania, Shedrack Msemo, alitaja miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo wakulima ni miundombinu mibovu ya kuingia kwenye mashamba ya wakulima, kutokuwa na mashine bora ya ukoboaji wa mpunga pamoja na mashine za kuvunia mpunga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako