• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kukabiliana na Marekani juu ya mikwaruzano yao ya kiuchumi na kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-05-11 18:01:22

    Mazungumzo ya duru ya 11 ya mambo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani yalimalizika Ijumaa huko Washington. Mwakilishi wa China katika mazungumzo hayo ambaye pia ni naibu waziri mkuu Bw Liu He aliwaambia wanahabari kuwa, pande mbili zilifanya mawasiliano ya dhati na kimkakati, na kukubaliana kufanya mazungumzo tena hapa Beijing katika siku za usoni na kuendelea kuhimiza mazungumzo kati yao.

    Bw. Liu alisema kuwa, kama Marekani ikipandisha kiwango cha ushuru wa forodha, lazima China itajibu. China haitaki kuona mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili ikipanda ngazi bila kikomo. Amefafanua kuwa uchumi wa China utaendelea kwa utulivu na kuwa mzuri na ingawa unakabiliwa na shinikizo, imani na matarajio ni muhimu sana.

    Hata hivyo amesema Marekani iliinyooshea kidole China kwa kutaka kujadiliana tena baadhi ya yaliyomo kwenye makubaliano, ikilenga kuifanya China ibebe lawama za kushindwa kwa mazungumzo, na kusisitiza kuwa hatua hiyo si ya haki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako