• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mwito wa kuwepo kwa ushirikiano na Marekani, kusema China haitayumba kwenye mambo ya msingi

    (GMT+08:00) 2019-05-12 18:23:53

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He amesema ushirikiano ndio njia pekee sahihi kwa China na Marekani, lakini China haitayumba kwenye mambo yake ya msingi.

    Akiongea na wanahabari baada ya kumalizika kwa duru ya 11 ya mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu uchumi na biashara kati ya China na Marekani, Bw Liu amesema uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, sio suala la nchi mbili tu, bali ni suala la amani ya dunia na maendeleo.

    Amesema China inapinga vikali kitendo cha Marekani kupandisha ushuru, ambacho sio tu kina madhara kwa Marekani na China, bali kina madhara kwa dunia nzima, na China itatakiwa kuchukua hatua za lazima za kujibu.

    Bw. Liu amesema makubaliano yoyote yanatakiwa kuwa na usawa na ya kunufaishana. Amesema tayari wamefikia makubaliano kwenye maswala mengi ya msingi, lakini bado kuna maswala matatu ya kimsingi yanayoitatiza China na ni lazima yashughulikiwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako