• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Libya lawaokoa wahamiaji haramu 147 kwenye pwani ya magharibi ya Libya

    (GMT+08:00) 2019-05-13 08:36:07

    Jeshi la majini la Libya limesema limewaokoa wahamiaji haramu 147 kwenye operesheni mbili tofauti zilizofanyika kwenye pwani ya Libya.

    Operesheni ya kwanza ilifanyika umbali wa maili 68 kwenye pwani ya mji wa Zawiya, ulioko kilometa 45 magharibi mwa mji wa Tripoli. Wahamiaji haramu 96 waliokolewa ikiwa ni pamoja na wanawake 16 na watoto wanne.

    Operesheni ya pili ilifanyika umbali wa maili 50 mashariki katika pwani ya mji wa Khoms, uliopo kilometa 120 mashariki mwa mji wa Tripoli, ambapo wahamiaji 51 waliokolewa.

    Wahamiaji hao wamepelekwa kwenye vituo vya kuwapokea baada ya kupatiwa msaada wa matibabu na kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako