• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo majaribio la utekelezaji wa mpango wa taifa wa China kuhusu mazingira ya asili lazinduliwa kisiwani Hainan

    (GMT+08:00) 2019-05-13 08:36:28

    China imezindua "utekelezaji wa mpango wa taifa kuhusu eneo la majaribio la mazingira ya asili katika kisiwa cha Hainan", kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa jumla wa mageuzi ya mfumo wa ustaarabu wa mazingira ya asili, kwenye kisiwa hicho kilichopo kusini mwa China.

    Waraka uliotolewa kwa pamoja na ofisi kuu ya kamati kuu ya chama cha Kikomunisti cha China na ofisi kuu ya baraza la serikali, imesema serikali italeta mtindo mpya wa kuishi kwa mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili, ikiwa ni sehemu za juhudi za China kuleta mambo ya kisasa na kufungua ukurasa mpya kwa Hainan kuijenga China bora.

    Baadhi ya mambo yatakayozingatiwa na eneo hilo, ni kuendeleza mfumo wa ustaarabu wa kiikolojia, utaratibu mzuri wa kugawa ardhi, na kuratibu maendeleo ya uhifadhi wa bahari na ardhi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako