• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yafungua tena vivuko viwili na ukanda wa Gaza baada ya kufungwa kwa siku 8

    (GMT+08:00) 2019-05-13 08:36:53

    Israel imefungua tena vivuko viwili na ukanda wa Gaza baada ya kufungwa kwa muda wa siku 8 kutokana na mvutano ulioibuka hivi karibuni kati yake ya makundi ya Palestina.

    Mamlaka za Israel zimeufahamisha upande wa Palestina kuwa imeamua kufungua vivuko vya Karem Shalom kusini mwa ukanda wa Gaza, na Erez katika upande wa kaskazini.

    Mbali na hilo, Ijumaa Israel ilitangaza kupanua ukanda wa uvuvi kwa maili 12 baharini, baada ya kupiga marufuku kwa siku sita, hatua ambayo imesema ni utekelezaji wa maelewano kutokana na makubaliano ya kusimamisha vita kati ya Israel na makundi ya Palestina.

    Misri, Qatar na Umoja wa mataifa wamefanikiwa kufikiwa kwa makubaliano ya kusimamisha vita kati ya Israel na makundi yenye silaha ya Gaza, baada ya kupambana kwa siku mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako