• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikosi vya Iraq vyaharibu vituo kumi vya maficho ya IS katikati ya nchi

    (GMT+08:00) 2019-05-13 08:39:31

    Vikosi vya usalama vya Iraq na wanamgambo wa Hashd Shaabi, wameharibu vituo kumi vinavyoaminiwa kuwa ni maficho ya wapiganaji wa kundi la Islamic State na kuwaua washambuliaji watatu wa kujitoa muhanga kwenye operesheni iliyofanyika Jumapili mkoani Salahudin, katikati ya nchi hiyo. Vikosi hivyo, vikiungwa mkono na helikopta za kivita, vilifanya shambulizi la ghafla dhidi ya wapiganaji wa Islamic State kwenye eneo la milimani la Himreen. Hali ya usalama nchini Iraq imeboreka kidhahiri baada ya vikosi vya usalama vya Iraq kupata ushindi kamili dhidi ya kundi la IS nchi kote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako