• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasimamia kuondoka kwa vikosi vya Houthi kutoka bandari tatu

    (GMT+08:00) 2019-05-13 08:44:18

    Tume maalumu ya Umoja wa Mataifa huko Hodeidah nchini Yemen, imetoka taarifa ikisema vikosi kazi vya Umoja wa Mataifa vimesimamia kuondoka kwa vikosi vya Houthi kutoka bandari tatu kuu ikiwemo Hodeidah, pia vitathibitisha rasmi hali ya kuondoa majeshi tarehe 14.

    Taarifa imesema, operesheni ya kuondoka kwa vikosi vya Houthi inachukuliwa kuwa ni hatua ya kwanza ya kutekeleza makubaliano ya kipindi cha kwanza, yaliyosainiwa kati ya waasi wa Houthi na serikali ya Yemen kuhusu kuondoa majeshi kutoka Hodeidah. Serikali ya Yemen pia imesema itatimiza ahadi kuhusu makubaliano hayo, wakati Umoja wa Mataifa utakapoitaka iondoe majeshi yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako