• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Utalii waimarika Tanzania.

    (GMT+08:00) 2019-05-13 18:15:48

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, anatarajiwa kupokea kundi la watalii 336 hii leo. Watalii hao watashiriki katika kongamano la Kimataifa la uwekezaji. Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Utalii (TTB), Devota Mdachi, anasema kwa watalii hao wanakuja kutangaza vivutio vilivyopo nchini kupitia mkakati unaofahamika kama Tour Africa New Horizon Visit to Tanzania. Watalii hao watakuwa nchini kwa siku nne na kutembelea hifadhi za taifa za Manyara na Serengeti, Bonde la Ngongoro . Olduvai Gorge na katika maeneo ya utalii wa utamaduni. Kongamano la Jumatatu la uwekezaji kati ya China na Tanzania litafunguliwa ba Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji). Watakaofaidika sana ni wafanyibiashara na wawekezaji wa kampuni zilizojikita katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za uimarishaji wa biashara ndogo na kati, utafiti na maendeleo, viwanda, utalii, utamaduni, ujenzi, nishati, mafuta na gesi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako