• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaombwa kutowapuuza wawekezaji wa kichina.

    (GMT+08:00) 2019-05-13 18:16:34
    SERIKALI imeshauriwa kutowapuuza wawekezaji wanaotoka China na kuja kuwekeza badala yake wawatumie kama daraja la kuweza kufikia malengo ya kuwa nchi yenye uchumi mkubwa duniani.

    Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, alipokuwa katika ghafla ya uzinduzi wa pombe kali aina ya Moutai ambayo kiwanda chake kipo China.

    Alisema pamoja na uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na China, lakini bado wameamua kutafuta kila mbinu ili kuweza kushirikiana katika masuala ya kiuchumi. Pinda alisema China ni taifa la pili kwa ukuaji wa uchumi duniani, hivyo hawapaswi kupuuzwa wanapokuja na mawazo yao ya kuanzisha biashara.

    Alisema wawekezaji wa China wameamua kutangaza biashara zao kubwa nchini, ikiwamo pombe hiyo ambayo ni maarufu China na nchi za Afrika Magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako