• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwanja mpya wa ndege wa Beijing washuhudia safari ya kwanza ya majaribio ya ndege za abiria

    (GMT+08:00) 2019-05-13 18:43:02

    Uwanja mpya wa kimataifa wa ndege wa Daxing ulioko mjini Beijing umemaliza jaribio lake la kwanza la safari ya ndege za abiria wakati ndege nne zilipotua salama leo asubuhi.

    Rubani mkuu wa Mamlaka ya Safari za Anga ya China Wan Xiangdong amesema, majaribio hayo yameonyesha kuwa uwanja mpya wa ndege umegeuza mwelekeo wake kutoka ujenzi wa miundombinu kuelekea maandalizi ya kutumika.

    Uwanja huo wa ndege unatarajiwa kuanza kutumika rasmi Septemba mwaka huu, na unatarajiwa kushughulikia abiria milioni 45 kwa mwaka itakapofika mwaka 2021.

    Ndege kutoka mashirika ya ndege ya China Southern, China Eastern, Air China na Xiamen Airlines zilitumika katika majaribio hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako