• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping: Ustaarabu tofauti yaifanya dunia iwe na mambo mengi

    (GMT+08:00) 2019-05-13 19:11:31

    Mazungumzo ya ustaarabu ya Asia yatafanyika mjini Beijing. Miaka mitano iliyopita, rais Xi Jinping alitoa hotuba katika makao makuu ya UNESCO na kusema kuwa, anapenda kuelewa ustaarabu tofauti wa mabara matano duniani. Katika miaka mitano iliyopita, rais Xi amezungumzia wazo lake kuhusu ustaarabu katika sehemu tofauti.

    Je, kwa nini rais wa China anatilia maanani sana ustaarabu, na kwa nini anapendekeza kufanya mazungumzo hayo ya ustaarabu? Hebu tutafute majibu kutokana na maneno yake.

    --Dunia ina nchi na sehemu zaidi 200, makabila zaidi 2,500 na dini mbalimbali. Historia na hali tofauti ya nchi, makabila na desturi tofauti, zinalea ustaarabu tofauti, ili dunia iwe na mambo mengi tofauti.

    --Ustaarabu mbalimbali wa binadamu ni sawa, zina umaalumu tofauti, pia zina upungufu wao wenyewe. Hakuna ustaarabu bila upungufu duniani, pia hakuna ustaarabu bila manufaa hata kidogo. Hakuna ustaarabu mzuri au mbaya.

    --Tofauti ya ustaarabu haipaswi kuwa chanzo cha mgogoro wa dunia, bali inapaswa kuwa motisha ya maendeleo ya ustaarabu wa binadamu.

    --China inapendekeza kufanya mazungumzo ya ustaarabu ya Asia, kuimarisha mawasiliano kati ya vijana, mashirika yasiyo ya kiserikali, vyombo vya habari na sekta mbalimbali, na kujenga mtandao wa ushirikiano na mawasiliano ya jumuiya ya washauri mabingwa, ili watu wa Asia wawe na maisha mazuri ya kiroho, na ushirikiano na maendeleo ya kanda hiyo uwe na uhai zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako