• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usalama wa chakula nchini China unaweza kuhakikishwa

    (GMT+08:00) 2019-05-13 19:28:16

    Mtaalam wa ngazi ya juu wa kilimo amesema, China inaweza kutimiza mahitaji muhimu ya kujitosheleza kwa nafaka na usalama wa chakula.

    Akizungumza leo kwenye jukwaa la sera za Kilimo la China na Jamii ya Kimataifa linalofanyika hapa Beijing, makamu rais wa Chuo cha Sayansi ya Kilimo cha China Bw. Mei Xurong amesema, upatikanaji wa chakula nchini China unaweza kuhakikisha ujenzi wa jamii yenye ustawi wa kati katika nyanja zote itakapofika mwaka 2020, na msingi wa kutimiza ujamaa wa kisasa ifikapo mwaka 2023.

    Ripoti ya "Maendeleo ya Sekta ya Kilimo 2019" iliyotolewa na Bw. Mei imeonyesha kuwa, mfumo wa chakula na kilimo umechangia asilimia 23.3 ya pato la taifa la ndani na asilimia 36.07 ya nafasi za ajira nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako