• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Upendo wa Xi Jinping kwa familia na taifa lake

    (GMT+08:00) 2019-05-13 20:28:32

    Kwenye mashelfu ya kuwekea vitabu vya rais Xi Jinping wa China, kuna picha nne kuhusu familia yake. Maisha ya furaha ya familia ni matumaini ya watu wa kawaida, pia ni matumaini ya rais Xi.

    Alipokuwa katibu wa baraza la Chama la mkoa wa Zhejiang, Xi aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kila siku alimpigia simu mke wake Peng Liyuan, ambaye alikuwa mwimbaji maarufu na kufanya maonesho mara kwa mara katika sehemu mbalimbali, na hii ilikuwa desuri yake iliyoendelea kwa miaka zaidi ya 10 tangu afunge naye ndoa.

    Tarehe 15, Oktoba mwaka 2001 ilikuwa siku ya 88 ya kuzaliwa kwa baba yake Xi, ambaye wakati huo alikuwa mkuu wa mkoa wa Fujian. Kutokana na kazi nyingi, alishindwa kuhudhuria karamu ya kusherehekea siku hiyo, akamwandikia babake barua ili kuomba msamaha.

    Mwaka 2015 katika tamasha la kuadhimisha sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, Xi alisoma shairi kuhusu wema wa mama, ambalo linajulikana na karibu wachina wote, nyuzi mkononi mwa mama, zinageuka kuwa nguo ya mtoto, anashona na anashona kabla ya kuagana, mama ana wasiwasi mtoto atachelewa kurudi. Alisema shairi hilo linaonesha upendo wa familia wa wachina.

    Tarehe 3 Februari mwaka huu, kwenye tamasha la kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina, rais Xi amesisitiza tena kuwa, ustawi na maendeleo ya taifa ni tegemeo la maisha ya furaha ya watu, na maisha ya furaha ya wananchi ni msingi wa ustawi na maendeleo ya taifa.

    Picha 1: Xi na mama yake

    Picha 2: Xi na baba yake pamoja na mke na mtoto wake.

    Picha 3: Xi na mke wake Peng Liyuan.

    Picha 4: Xi na mtoto wake.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako