Bei ya maharage ya soya kwa mauzo ya baadaye kwenye Bodi ya biashara ya Chicago imefikia kiwango cha chini zaidi katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 iliyopita, kutokana na wasiwasi wa wafanyabiashara kuhusu kupamba moto kwa mgogoro wa kibiashara kati ya Marekani na China. China imetangaza kuwa itaongeza kiwango cha ushuru dhidi ya baadhi ya bidhaa za Marekani kuanzia Juni mosi. Uamuzi huo umekuja baada ya Marekani kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 200 kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kuanzia Mei 10.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |