• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China, Russia na Marekani zinapaswa kufanya juhudi za pamoja katika kuleta utulivu na maendeleo duniani

    (GMT+08:00) 2019-05-14 09:36:56

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China, Russia na Marekani zinapaswa kuendelea kupanua ushirikiano, na kutoa mchango kwa pamoja kwa ajili ya utulivu na maendeleo ya dunia.

    Akizungumza na wanahabari baada ya kukutana na mwenzake wa Russia Bw. Sergei Lavrov, Bw Wang amesema China, Russia na Marekani zikiwa ni wajumbe wa kudumu wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, zinapaswa kuwasiliana na kushirikiana ili kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili dunia kwa sasa.

    Amesisitiza kuwa nchi hizo tatu zinahitaji kuondoa mashaka yasiyo ya lazima, na kuendelea kupanua ushirikiano, ili kulinda amani na utulivu wa dunia na kuhimiza maendeleo na ustawi wa dunia. Ameongeza kuwa uhusiano kati ya China na Russia umetoa mfano mzuri kwa jumuiya ya kimataifa. Pia China inapenda kuondoa tofauti kwenye msingi wa kuheshimiana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako