• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya biashara kati ya China na Marekani yapaswa kufanyika katika msingi wa usawa

    (GMT+08:00) 2019-05-14 19:15:50

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, China na Marekani zinapaswa kufanya mazungumzo ya kibiashara katika msingi wa usawa, badala ya kulaumiana na kuweka shinikizo dhidi ya upande mwingine wakati wa mchakato wa majadiliano.

    Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Taifa wa China, amesema hayo alipokutana na waandishi wa habari mjini Sochi, Russia, baada ya kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo, Sergey Lavrov. Amesema China na Marekani zimepata maendeleo dhahiri kupitia juhudi zao za pamoja, lakini bado kuna mambo yanayotakiwa kushughulikiwa kwa makini na kutatuliwa.

    Wang amesisitiza kuwa majadiliano sio njia ya upande mmoja lakini yanapaswa kuchukuliwa katika msingi wa usawa, akisema ni vigumu kutegemea upande mmoja kukubali kirahisi maombi ya upande mwingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako