• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China aanzisha CDAC kuboresha mabadilishano ya kiutamaduni

    (GMT+08:00) 2019-05-14 19:22:42

    Mjumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Bw. Huang Kunming amesema, mkutano ujao wa mazungumzo ya ustaarabu wa Asia (CDAC) uliopendekezwa na rais Xi Jinping wa China, unalenga kujenga jukwaa kwa nchi za Asia kuwasiliana, kubadilishana maoni na kuonyesha utamaduni wao.

    Bw. Huang amesema hayo alipokutana na makamu mwenyekiti wa Bunge la Mongolia, L. Enkh-Amgalan, ambaye yuko hapa Beijing kuhudhuria mkutano huo. Amesema mkutano huo utakuwa tukio kubwa katika historia ya mabadilishano kati ya ustaarabu wa Asia na wa dunia.

    Amesema anatumai kuwa China na Mongolia zitaendeleza mawasiliano ya watu na pia utamaduni ili kuimarisha uungaji mkono wa umma wa ushirikiano wa kimakakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

    Kwa upande wake, Enkh-Amgalan amesema, Mongolia iko tayari kufanya kazi na China kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, uchumi, na utamaduni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako