• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi kuu Tanzania Bara – Yanga yaishusha Simba, yarejea kileleni mwa ligi

  (GMT+08:00) 2019-05-15 09:19:47

  Yanga SC ya Dar es Salaam, imerejea tena kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting jana jioni uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

  Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe alama 83 baada ya kucheza mechi 36, sasa inawazidi alama moja watani wao wa jadi Simba SC ambao hata hivyo wana mechi tatu mkononi.

  Bao pekee la Yanga lilifungwa na mchezaji wa kimataifa wa DRC Pappy Tshishimbi dakika ya 15 ya mchezo.

  Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Mwadui FC imelazimishwa sare ya goli 3-3 na jirani zao Mbao FC.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako