• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fainali ya mabingwa Afrika 2019- Wydad Casablanca na Esperance de Tunis

    (GMT+08:00) 2019-05-15 09:20:07
    Wababe wawili kutoka kaskazini mwa Afrika, Esperance de Tunis kutoka Tunisia na Wydad Casablanca ya Morocco, watamenyana katika kipute cha fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika ya mwaka huu 2019, mchezo utakaopigwa mwishoni mwa mwezi huu.

    Wydad Casablanca wataanzia nyumbani kuwaalika Esperance de Tunis katika fainali ya kwanza Mei 24 kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdallah mjini Rabat, Morocco kabla ya Esperance de Tunis kuwakaribisha Wydad Casablanca kwenye mechi ya marudiano Mei 31 katika uwanja wa Olimpiki mjini Rades, Tunisia.

    Klabu hizo zimetinga fainali hiyo kwa kukatiza safari za TP Mazembe ya DRC na Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako