• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michuano ya wazi ya Italia- Williams na Wozniacki wajitoa kutokana na kuwa majeruhi

    (GMT+08:00) 2019-05-15 09:20:26
    Bingwa mara 23 wa tenisi duniani Serena Williams amejiondoa katika michuano ya tenisi ya wazi ya Italia kutokana na kuumia goti, lakini amesema atashiriki michuano ya wazi ya Ufaransa, Serena alipangwa kukutana na dada yake Venus Williams katika hatua ya pili lakini mchezo huo umeshindikana kutokana na kuwa majeruhi.

    Naye bingwa wa zamani wa dunia wa mchezo huo, Caroline Wozniacki naye ameondolewa katika michuano hiyo, baada ya kuumia katika mchezo wake wa kwanza na Danielle Collins ambapo alipoteza kwa seti 7-6 na 7-5.

    Michuano ya wazi ya tenisi ya Ufaransa itaanza kutimua vumbi Mei 23.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako