• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa Waraka wa Mapendekezo kuhusu Mageuzi ya WTO

    (GMT+08:00) 2019-05-15 09:58:35
    Habari kutoka Wizara ya biashara ya China zimesema, China imewasilisha Waraka wa Mapendekezo kuhusu Mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani WTO kwenye shirika hilo. Ofisa wa wizara hiyo amesema China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali ili kusukuma mbele kwa pamoja mageuzi hayo, na kuhimiza shirika hilo lichangie zaidi katika usimamizi wa mambo ya uchumi duniani.

    Mkurugenzi wa Kitengo cha mambo ya WTO katika wizara hiyo ameeleza kuwa mapendekezo yaliyotolewa na China yanahusisha maeneo manne muhimu yakiwa ni pamoja na kutatua masuala makuu yanayotishia uwepo wa shirika hilo; kuihusisha zaidi WTO kwenye usimamizi wa mambo ya uchumi duniani; kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa WTO, na kuongeza ushirikishi wa utaratibu wa biashara ya pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako