• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mazungumzo ya staarabu za Asia wafunguliwa Beijing

    (GMT+08:00) 2019-05-15 10:45:40

    Mkutano wa mazungumzo ya staarabu za Asia umefunguliwa leo hapa Beijing, na rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba.

    Wakuu wa nchi na serikali kutoka Combodia, Ugiriki, Singapore, Sri Lanka na Armenia, viongozi wa Mongolia na wakuu wa mashirika ya kimataifa likiwemo Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO wamehudhuria mkutano huo.

    Mkutano wa mazungumzo ya ustaarabu wa Asia una kauli mbiu ya "mawasiliano na kufundishana kwa staarabu za Asia na mustakbali wa pamoja", na umehudhuriwa na vijana, wasomi, maofisa wa serikali kutoka nchi 47 za Asia na za nchi nyingine zisizo za Asia pamoja na wajumbe wa mashirika ya kimataifa. Mbali na mkutano wa ufunguzi, makongamano, tamasha la utamaduni wa Asia, wiki ya utamaduni wa Asia pia itafanyika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako