• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asema kubaliana na changamoto za dunia nzima kunahitaji nguvu ya utamaduni na ustaarabu

    (GMT+08:00) 2019-05-15 11:15:01

    Mkutano wa mazungumzo ya ustaarabu wa Asia leo umefunguliwa hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba akisema, binadamu wanapokabiliana na changamoto za pamoja, sio tu wanatakiwa kuwa na nguvu ya kisayansi na kiuchumi, bali pia wanatakiwa kuwa na nguvu ya utamaduni na ustaarabu.

    Rais Xi amesema, hivi sasa dunia yenye ncha nyingi, utandawazi wa uchumi duniani, utamaduni wa aina nyingi na untadawazi wa upashanaji habari kwenye jamii unaoendelea kwa kina, yote hayo yameleta matumaini makubwa kwa jamii ya binadamu. Lakini amedhihirisha kuwa hali isiyo na utulivu na uhakika imeonekana kuwa ni dhahiri zaidi, changamoto zinazowakabili binadamu wote inazidi kuwa kubwa zaidi. Anaona kuwa mkutano huo umetoa jukwaa jipya kwa kuhimiza nchi za Asia na nchi nyingine duniani mbalimbali zifanye mazungumzo wenyenye usawa kuhusu ustaarabu, kuingiliana na kufundishana, ili kila upande uweze kupata mwanga mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako