• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asema China ya hivi leo ni China ya Dunia

    (GMT+08:00) 2019-05-15 12:12:19

    Rais Xi Jinping wa China leo ametoa hotuba kwenye mkutano wa mazungumzo ya ustaarabu wa Asia ikisema, China ya hivi leo sio tu ni nchi ya China, bali pia ni China ya Asia na China ya Dunia.

    Rais Xi amesema, ustaarabu wa China ni sehmu muhimu inayounda ustaarabu wa Asia. Tangu enzi na Dahari, ustaarabu wa China unakua siku hadi siku katika mchakato wa kurithi na kufanya uvumbuzi, na kujiinulia kiwango wakati wa kukabiliana na mabadiliko yaliyotokea kila wakati, huku ukiendelea kuongeza utafutaji wake wa kiroho wa taifa la China. Ustaarabu wa Taifa la China siku zote unaonekana kuwa na nguvu mpya ya uhai katika mchakato wa kuingiliana na mambo mbalimbali tofauti. Kuishi pamoja kwa amani na nchi jirani, kushirikiana kwa amani na nchi mbalimbali duniani ni wazo la uwepo wa ustaarabu wa China, na kuwanufaisha watu na kuwafanya waishi maisha yenye usalama na utajiri ni mwelekeo wa thamani ya ustaarabu wa Taifa la China. Kufanya mabadiliko na kuenda na wakati ni moyo wa daima milele wa ustaarabu wa China, huku kuheshimu maumbile na kuishi pamoja na mazingira ya asili kwenye hali ya kupatana kukiwa wazo la uwepo wa ndani wa ustaarabu wa Taifa la China.. Rais Xi ameeleza imani kuwa China ya siku za baadaye hakika itazifungulia mlango nchi za nje na kutoa mchango mkubwa kwa dunia kwa mafanikio yake ya ustaarabu yenye uhai zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako