Kakunda alisema Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi ili kuhakikisha wadau wote wanatoa mchango unaohitajika katika ujenzi wa uchumi wa Taifa. Alisema pamoja na mazingira rafiki ya uwekezaji katika viwanda na biashara, utekelezaji wa mpango wa kuboresha mazingira ya biashara (blue print) unaangaliwa kuwa sehemu ya tiba ya changamoto ambazo zinaitatiza sekta binafsi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |