• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachukua nafasi ya kwanza katika kuwekeza kwenye sekta ya nishati

    (GMT+08:00) 2019-05-15 17:27:22
    Ripoti ya uwekezaji wa sekta ya nishati ya mwaka 2019 iliyotolewa na Shirika la Nishati la Kimataifa imesema, thamani ya uwekezaji wa nishati dunianikwa mwaka jana imefikia dola za Marekani trilioni 1.8 ambapo China imechukua nafasi ya kwanza.

    Ripoti hiyo imesema, thamani ya uwekezaji wa sekta ya nishati ya China kwa mwaka jana ilifikia dola za kimarekani bilioni 381 ambayo imepita Marekani kwa dola za Marekani bilioni 30. Nchi iliyoongeza uwekezaji kwa wingizaidi kwenye sekta hiyo ni Marekani ambayo ongezeko lake lilifikia dola za Marekani bilioni 17.

    Mkuu wa shirika hilo Bw. Fatih Birol amesema, hivi sasa, uwekezaji katika sekta hiyo bado haujakidhi mahitaji ya mfumo wa matumizi. Pia uwekezaji wa nishati safi bado ni mdogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako