• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China umeendelezwa katika kiwango kichachofaa katika mwezi Aprili mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-05-15 18:37:47

    Msemaji wa idara ya takwimu ya China Bibi Liu Aihua leo hapa Beijing amesema katika mwezi Aprili mwaka huu, uchumi wa China umeendelezwa katika kiwango kinachofaa, hali ya uendeshaji wa uchumi ni tulivu kwa ujumla, na umeongezeka kwa madhubuti.

    Katika mwezi huo, sekta ya huduma imeongezeka kwa kasi, uzalishaji wa viwanda umeendelea kwa utulivu, na ongezeko la sekta mpya za viwanda na bidhaa mpya ni la kasi. Takwimu zinaonyesha kuwa, kiwango cha uzalishaji wa sekta ya huduma katika mwezi Aprili kimeongezeka kwa asilimia 7.4 kuliko mwaka jana wakati kama huo.

    Aidha, kasi ya ongezeko la uuzaji wa bidhaa nchini China imepungua, huku biashara ya rejareja kwenye mtandao wa Internet ikiongezeka kwa kasi. Uwekezaji umedumisha ongezeko kwa utulivu, na uwekezaji katika sekta ya teknolojia ya juu umeongezeka kwa kasi. Biashara ya uuzaji wa bidhaa kwa nje na uagizaji bidhaa kutoka nje imeendelea kuongezeka, na muundo wa biashara umeendelea kuboreshwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako