• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Andrea Bocelli kuimba kwenye maonesho ya utamaduni wa Asia

    (GMT+08:00) 2019-05-15 18:57:54

    Bw. Andrea Bocelli anayejulikana kama mwimbaji wa nne mwenye sauti ya juu zaidi duniani ataimba leo usiku hapa Beijing kwenye maonesho ya utamaduni wa Asia.

    Bw. Bocelli amesema anafurahi kuona China na Italia zinaongeza mawasiliano ya utamaduni na muziki katika miaka ya hivi karibuni. Amesema aliwahi kushirikiana na wanamuziki wengi wa China, na muziki wao umemwachia kumbukumbu nzuri.

    Akizungumzia mawasiliano ya ustaarabu, amesema mawasiliano hayo ni muhimu sana, na kuongeza kuwa muziki ni lugha ya kimataifa, ambayo inaweza kuhimiza maelewano kati ya watu wenye tamaduni tofauti, na kuimarisha msingi wa amani, utulivu na masikilizano duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako