• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ustaarabu wa China wasaidia kuhimiza nchi za Asia kupata maafikiano kwenye mchakato wa maendeleo

    (GMT+08:00) 2019-05-15 19:28:11

    Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Shirika la Ustaarabu la Umoja wa Mataifa Bw. Miguel Angel Moratinos amesema ustaarabu wa China unasaidia kuhimiza nchi za Asia kupata maafikiano kwenye mchakato wa kutafuta maendeleo ya jamii na uchumi.

    Akizungumza hivi karibuni kwenye Makao Makuu ya Umoja huo mjini New York, Bw. Moratinos amesema, ustaarabu wa China ambao ni moja ya ustaarabu mkuu zaidi duniani umetoa mchango mkubwa kwa kupanda na kuendelea kwa ustaarabu wa binadamu, na pia umeathiri ustaarabu wa bara la Asia kwa kiwango kikubwa.

    Bw. Moratinos anaamini kuwa, kwa kupitia mawasiliano na mazungumzo kati ya ustaarabu tofauti za nchi za Asia, ikiwemo mazungumzo ya Ustaarabu ya Asia yanayofanyika hapa Beijing, bara la Asia lenye matumaini mazuri litafikia mustakabali nzuri zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako