• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madai ya Marekani kuwa wateja wake hawataathiriwa na hatua ya kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China, hayana msingi

    (GMT+08:00) 2019-05-16 08:49:29

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, madai ya Marekani kuwa wateja wake hawataathiriwa na hatua ya kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China, hayana msingi, na China inaitaka Marekani itambue hali halisi, kurudi kwenye njia sahihi na kwenda sambamba na China.

    Bw. Geng Shuang amesema katika miaka kadhaa iliyopita, China imekuwa mteja mkubwa wa bidhaa za kilimo za Marekani. Mwaka 2017 asilimia 60 ya maharage ya soya ya Marekani yaliuzwa China, lakini mauzo hayo yamepungua kwa kiasi kikubwa baada ya Marekani kuzusha mgogoro wa kibiashara dhidi ya China.

    Msemaji huyo pia amesema ripoti ya utafiti uliofanywa na wachumi wa Marekani inaonesha kuwa, hatua ya Marekani kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China imewasababishia wateja na waingizaji bidhaa kutoka nje wa Marekani hasara ya dola bilioni 4.4 za kimarekani kila mwezi.

    Bw. Geng Shuang amesema Marekani inatakiwa kutambua hali halisi, kurejea mapema kwenye njia sahihi na kwenda sambamba na China, ili pande hizo mbili ziweze kufikia makubaliano kwenye msingi wa kuheshimiana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako