• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa UM wazihimiza pande hasimu za Yemen kuhimiza ufumbuzi wa kudumu wa kisiasa

    (GMT+08:00) 2019-05-16 08:50:16

    Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Bw. Martin Griffiths amezitaka pande hasimu nchini Yemen ziweke kando tofauti zao na kuhimiza ufumbuzi wa kudumu wa kisiasa wa mgogoro kati yao.

    Akiongea kwenye mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuhusu Mashariki ya Kati, Bw. Griffiths amesema "mabadiliko yametokea mjini Hodaidah" baada ya vikosi vya waasi wa Houthi kuanza kuondoka kutoka kwenye bandari za Hodeidah, Saleef na Ras Issa, chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa kati ya Mei 11 na 14.

    Bw. Griffiths ameyataja maendeleo hayo kama "hatua ya kwanza kuelekea utekelezaji wa makubaliano ya Hodeidah" yaliyofikiwa Disemba mwaka 2018 mjini Stockholm.

    Mjumbe huyo pia ametahadharisha kuwa licha ya maendeleo yaliyopatikana katika siku kadhaa zilizopita, Yemen bado iko kwenye njia panda kati ya vita na amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako