• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Afrika Kusini aahidi kuanzisha mageuzi ya kiuchumi

  (GMT+08:00) 2019-05-16 09:27:34

  Kufuatia ukuaji wa polepole wa uchumi na ukosefu wa nafasi za ajira, rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema katika mkutano wa wawekezaji wa Goldman Sachs kuwa serikali yake itatilia maanani mageuzi ya kiuchumi ili kufungua fursa za kiuchumi na kuleta ajira.

  Akizungumza na mkurugenzi mtendaji mkuu wa shirika la Goldman Sachs Kanda ya Afrika kusini mwa Sahara Bw. Colin Coleman, rais Ramaphosa amesema jambo la kwanza la kurekebisha uchumi ni kutatua matatizo mengine makubwa.

  Rais huyo amesema, changamoto kubwa ni kiwango cha chini cha ukuaji wa uchumi, na kila kitu kinahusiana na uchumi, lakini kwanza kabisa inatakiwa kutatua suala la ajira.

  Tangu rais huyo achaguliwe kuwa mwenyekiti wa chama cha ANC, wachumi wamesema kuwa Afrika Kusini inatakiwa kuweka bayana msimamo wake kisera. Rais Ramaphosa amesema, uhakika wa sera ni muhimu katika kuwavutia wawekezaji na kushughulikia vizuizi vingine vya uwekezaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako