• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la kijeshi la Sudan lasimamisha mazungumzo na upinzani kwa saa 72

  (GMT+08:00) 2019-05-16 10:37:56

  Baraza la mpito la kijeshi la Sudan limetangaza kusimamisha kwa muda wa saa 72 mazungumzo kati yake na makundi makubwa ya upinzani.

  Mwenyekiti wa baraza hilo Abdel-Fattah Al- Burhan ametoa taarifa kwa njia ya televisheni akisema mazungumzo hayo yamesitishwa hadi mazingira yakiandaliwa kwa ajili ya mazungumzo hayo.

  Bw Al-Burhan ameweka masharti ya kurudisha tena mazungumzo hayo kuwa ni kuondoa vizuizi vilivyowekwa na waandamanaji nje ya maeneo wanayokaa, kufungua reli na kuzuia uchochezi kupitia vyombo vya habari, na kuacha kuwanyanyasa wana usalama.

  Pia ameyashutumu makundi yenye silaha kujipenyeza kwa waandamanaji wanaokaa na kuwalenga wana usalama.

  Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya baraza la kijeshi kufikia makubaliano na upinzani kuhusu muda wa mpito na madaraka ya idara za utawala.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako