• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani yanapaswa kuwa na udhati

    (GMT+08:00) 2019-05-16 19:48:27

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo amesisitiza kuwa, mazumgumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani yanapaswa kuwa na udhati.

    Bw. Lu Kang amesema, katika mambo ya kimataifa, China siku zote inatetea kutatua migongano kwa njia ya mazungumzo. Kuhusu masuala yanayotokea kwenye uhusiano wa uchumi na biashara kati ya China na Marekani, China pia inaona kuwa mazungumzo ndio njia sahihi ya kutatua masuala.

    Amesema China inasisitiza mambo mawili, pande mbili za mazungumzo zinapaswa kuheshimiana na kunufaishana kwa usawa, na ni lazima ziwe na uaminifu na kufuata maamuzi yanayofikiwa na pande hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako