• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WAVU: Kikosi cha Malkia Strikers kitakachokwenda Kampala chatajwa

    (GMT+08:00) 2019-05-17 09:55:18

    Mabingwa wa Voliboli ya wanawake barani Afrika ya mashindano ya All-Africa, Kenya wametaja kikosi cha wachezaji 12 kinachowania tiketi ya kutetea taji katika mchujo wa ukanda wa tano jijini Kampala, Uganda Mei 18-25, 2019.

    Timu ya Kenya, ambayo imekuwa ikifanyia mazoezi yake katika ukumbi wa kimataifa wa Kasarani, inatarajiwa kuelekea nchini Uganda leo Ijumaa kwa mashindano hayo ambayo mshindi atafuzu kushiriki makala hayo ya 12 mjini Rabat nchini Morocco. Nchini Uganda, Kenya itakutana na wenyeji Uganda, mahasimu wa tangu jadi Misri pamoja na Rwanda, Tanzania na Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako