• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Huawei yazindua simu za teknolojia ya 5G nchini Uingereza

    (GMT+08:00) 2019-05-17 17:21:35

    Kampuni ya Huawei ya China imezindua simu ya mkononi inayotumia teknolojia ya 5G nchini Uingereza, na mashirika yanayotoa huduma ya 5G yanatarajiwa kuanza kutumia mtandao wa 5G. Simu hiyo mpya aina ya Huawei Mate 20X itaanza kuuzwa mwezi ujao.

    Wakati hilo linajiri nchini Uingereza, kampuni ya Huawei imepinga uamuzi wa Idara ya Viwanda na Usalama ya wizara ya biashara ya Marekani, kuiweka kampuni ya Huawei kwenye orodha ya makampuni ambayo wamarekani wanazuiwa kuuza au kusafirisha teknolojia. Taarifa iliyotolewa na kampuni ya Huawei inasema uamuzi huo hauna maslahi kwa upande wowote, na utayaathiri makampuni menbgi yanayofanya biashara na kampuni ya Huawei, kuathiri nafasi nyingi za ajira za wamarekani, na kuharibu ushirikiano na kuaminiana kulikopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako