• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkopo mpya wa Eurobond kuzidi kuumiza wananchi

    (GMT+08:00) 2019-05-17 18:55:40
    Hatua ya serikali ya Kenya kuchukua mkopo mpya wa Eurobond Alhamisi ilisababisha hamaki kwa Wakenya wengi wanaohofia itaendelea kusababisha hali ngumu ya maisha kwa wananchi.

    Takwimu za Benki Kuu ya Kenya zinaonyesha kufikia Septemba 2018, Kenya ilikuwa na madeni ya jumla ya Sh5.1 trilioni, ambazo zimekopeshwa kutoka kwa wawekezaji wa humu nchini na mataifa ya kigeni yakiongozwa na Uchina.

    Mkopo mpya wa Eurobond wa Sh210 bilioni, ambao ni wa tatu kuchukuliwa tangu Rais Uhuru Kenyatta alipoingia mamlakani mnamo 2013, umesababisha madeni ya taifa hilii kuongezeka zaidi.

    Hii inamaanisha sasa ikiwa Wakenya wote karibu milioni 45 watahitajika kuchangia malipo ya mikopo iliyopo, kila mmoja atatakikana kugharamia zaidi ya Sh117,000.

    Kulingana na serikali, Sh75 bilioni kutoka kwa fedha hizo zitatumiwa kulipa madeni machache ya awali.

    Waziri wa Fedha, Bw Henry Rotich alisema mbali na kutumiwa kulipa baadhi ya madeni yaliyochukuliwa awali, mkopo huo utagharamia miradi kadhaa ya miundomsingi na mahitaji mengine kwenye bajeti ya taifa ambayo imepangiwa kusomwa mwezi ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako