• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Teknolojia pekee ndiyo itaokoa bara la Afrika – Rais

    (GMT+08:00) 2019-05-17 18:56:20
    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa wito kwa nchi za Afrika kuupa kipaumbele ushirikishi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) katika mipango yao ya maendeleo kwani fani hiyo ina uwezo mkubwa wa kuimarisha uchumi wa mataifa hayo.

    Rais alisema haya alipozindua mpango wa taifa la Kenya wa kustawisha uchumi kwa kutumia mfumo wa dijitali kwa wawekezaji na viongozi wa mataifa wanaohudhuria mkutano wa mwaka huu wa kuchochea mageuzi barani Afrika, uliofanyika jijini Kigali, Rwanda. Mpango huo unatambulika kimombo kama; "Smart Africa Initiative"

    Viongozi wa mataifa waliohudhuria uzinduzi huo ni mwenyeji; Rais Paul Kagame na Rais wa Mali, Boubakar Keita. Rais huyo wa Rwanda ndiye mwenyekiti sasa wa mpango huo unaolenga kubuni soko moja la kidijitali katika bara hilo kufanikisha biashara na uwekezaji.

    Mkakati wa kidijitali wa taifa la Kenya chini ya mada, "Kuthibiti Uwezo wa Mabadiliko nchini Kenya" ulizinduliwa mbele ya zaidi ya wajumbe 4,000 miongoni mwao maafisa wa serikali, watunga sera na maongozi, wabunifu na wawekezaji katika nyanja ya tekniolojia ambao wanakutana kujadili jinsi raslimali za ICT zinazvyoweza kutumika kuimarisha uchumi wa mataifa ya Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako